Skip to main content

Posts

To The Man I Love.

TO THE SOUL

  Istock.com Dear soul… Today, I want to talk to you. It really pains me, seeing how much you’re suffering, in distress, pain, agony, depression over matters that are out of your control. You have failed me so many times when you almost gave up and thought as though no one sees your sufferings. Don’t you believe that all that we go through is by the decree of our creator? I know you do know that everything that happens was long planned by the master of planners. Then why waste plenty of your precious time worrying over Allah’s decree. He knows you much more better than you do to your own self. How about live a worry-free and hope-full life acknowledging that everything is in control? If life was only made of good days, we would never learn to appreciate it, we would never know how it feels to be really Joyous. It’s the bad days that make us stronger, they make us more humble and adds up to our gratitude, because life, is made of two days; one is for you, and one against you. Learn ...
Recent posts

CHISA WARI WA HARUSI

Istockphoto.com Myawenu nfwitsani, mana mairo nkedza, Nazoreswa nfulani, dzina sitaki riadza, Nkadudula vueni, zikanihasiri todza, Chisa wari wa harusi, Yeya nkakatwa mala. Aredza nkamuona, nphisa asinichape, Mchengechenge ye bwana, asiime aphatsape, Amani chiphahikana, habari zosi nkupe, Chisa wari wa harusi, Yeya nkakatwa mala. Naphaha simu ya Mwari, kuna harusi ko kpwao, "Ndzoo nkupe wari, na usedze na myao," Chilaga nine wa Tari, "nenda ndoani mwenzio," Chisa wari wa harusi, Yeya nkakatwa mala. Ayangu kondze akala, mi chumbani chiphiripkwa, Chichekani chisagala, ko konze atu npkwapkwa, Sidzangbwe enda salala, sahani hino chiipkwa, Chisa wari wa harusi, Yeya nkakatwa mala. Mikono yangu yagbwirwa, ichisuwiwa vinono, Amba mwenye naererwa, nchigachenula meno, Gafula uchimenyerwa, na dzilume ra dzikono, Chisa wari wa harusi, Yeya nkakatwa mala. "Huyu ni nani we Mwari, haimjui famili? Hiye bwana ni hatari, watsomola rumu kali, Phahi nakakama mwiri, chinangamika a...

NIFANYEJE?

pixabay.com free images  Ndugu zangu nawaomba, mwenzenu 'saidieni, Mana nishagonga mwamba, sijui nifanye nini, Dau langu linayumba, lataka zama majini, 'Limpenda kanikana, sasa anitaka tena. 'Limpenda kanikana, sasa anitaka tena, Na nilipata kimwana, wenyewe tunaendana, Mtoto mzuri sana, wa kumzidi hakuna, Ila naye ni kicheche, wengi wanamtambua. Ila naye ni kicheche, wengi wanamtambua, Hatembei na wachache, penzini hajatulia, Hunichoma kama cheche, moyoni nikaumia, Ila nataka mfunza, huenda akageuka. Ila nataka mfunza, huenda akageuka, Mana vyema hunitunza, hadi nikafurahika, Na huyu mwingine mwenza, tabia 'mekamilika. Tatizo alinigura, wakati 'lipomtaka. Tatizo alinigura, wakati 'lipomtaka, Ninahisi ufukara, ndo chanzo cha kunepuka, Kwa sasa nami nang'ara, ndio kwangu achipuka, Amekuja kuniomba, nimpe wangu mtima. Amekuja kuniomba, nimpe wangu mtima, Kweli ilopo ni kwamba, mamboye yote ni mema, Janga linalonikumba, nitamwacha nani nyuma? Mana yeye yu kamil...

BRIDGING THE AGE GAP THROUGH CONSERVATION

A photo showing members of Kwale Pen People, Kwale Arts, SHIFOGA and Wazee wa Kaya preparing the field for tree planting.  DEMYSTIFYING THE TERM KAYA.  (Episode 1 of the story telling sessions)  Adigo Similani! We’re approaching Kaya Nimwache in the  Ziani ((Ziwani) area of  Matuga sub-county and our stupid conversations cut short by the field in front of us, popularly known as Bingo. A lot of local soccer matches happen here I’m told, this is my first time and I honestly feel attacked because whoever is leading the way wasn’t born neither did he spend the first 19 years of his life around this area. Anyway, we walk our way through past the “soccer field” into a swampy field to the other side (I really wish I was good at directions) where the rest of the participants in this program are. Talking about the program, BRIDGING THE GAP, is a program with the aim of narrowing the gap between the youth and the elderly in the society. The first phase being tree planting...

Uwiko wa kokoiko

Koo mwakorikoko,wiko jogoo huwika Hunadi kwa kokoiko,mnadi wa kuamka Koriko lake tamko,mawio ndo husikika Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika Koo wendako siko,kung'ang'ania kuwika Si swifa yako uwiko,sauti vunja mbarika Wasulubu Koo yako,na wiko halitotoka Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika Koo lako kokoreko,mjuzi kukokoreka Hukoreka kwa kereko,mwewe akishafika Ila hili kokoiko,si lako Koo kanyika Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika Koo mfanoo koko,kizazi unakiweka Ni tunu ya mola wako,Qahari alotukuka Keshakugawia lako,mbona hutaki ridhika? Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika E Koo swirati yako,njia iliyonyooka Pepo ikupelekako,kwenye mandhari tukuka Siri yake ni ridhiko,moyo wako kutosheka Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika Wasalamu nenda huko,kuliko waloridhika Wale waso unguliko,la inadi ya kuwika Waelewao tamko,tukufu lake rabuka Uwiko wa kokoiko,Koo si wako bazika ©May 26 200 M.J.Mwinyi mwinyimwaphatsa@gmail.com #Anti- feminism

Unani ka huna una?

Mvuvi ahanahana,uwerevu umemwisha Pakacha haloni tena,mzigo wa kujitwisha Ahangana kila kona,samaki kiwazungusha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Kutwa ameuza sina,una hana wameisha Waliisha toka Jana,pakachale kuliosha Na wateja megandana,ka huna una pitisha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Leo kutoka mchana,Sasa jua linkwisha Ameuza kwa Amina,kiuzo cha kukopesha Afanyeni ana wana,anataka kuwalisha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Wateja kina Shaina,kupara kumewachosha Vidole vi tele hina,sangara atamwangusha Ndiposa wataka una,rahisi kumchemsha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Wavuvi woga wa kina,wavivu nyavu kurusha Huwapapatia una,madebe kuyafungasha Kisa wapo juu sana,hawenzi kujitabisha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Una hata ladha hana,sekunde kukinaisha Ni ja ng'onda hajanona,minofu kujipwatisha Hata paka akimwona,hamli anampisha Unani ka huna una?ndo swali lilomchosha Ashangaa akiona,una wakimuitisha Wakimpangia vina,na taji wakamvisha ...

MCHUZI WA PWEZA

Nalianza tungo langu, kwa maswali kutatiza, Utamu moyoni mwangu,  kama nimepata viza, Nitapiga mtu rungu, ukweli atoliweza, KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU. Nawala sitatatiza, wala kuchoka mbioni, Maswala sitauliza, nitayajibu mwishoni, Nitapita kwenye kiza, ingawa mimi sioni, KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU.  Mwenyewe nitakubali, na kifua kujipiga, Hakika Mimi rejali, popote pale 'navyoga' Simi dume suruwali, nimeondoa uoga, KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU. Nguvu zote zi mwilini, hadi  zile za ziada Bora niwe kwa makini, niutowe ushuhuda Uridhike kwa mizani, uzito silete shida, KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU. Hichi kipya cha walili, watatu ufaidini, Nitaufanya ukali, asibaki mlangoni, Nyuki nile na hasali, juu wala sio chini, KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU  Wakufumbua fumbua, lengo lidhiirike, Watu pate yatambua, kila moja shike yake, Mi mgongo nananyua,  mwenyewe nipatoreke, KUMBE M...