Nalianza tungo langu, kwa maswali kutatiza,
Utamu moyoni mwangu, kama nimepata viza,
Nitapiga mtu rungu, ukweli atoliweza,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU.
Nawala sitatatiza, wala kuchoka mbioni,
Maswala sitauliza, nitayajibu mwishoni,
Nitapita kwenye kiza, ingawa mimi sioni,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU.
Mwenyewe nitakubali, na kifua kujipiga,
Hakika Mimi rejali, popote pale 'navyoga'
Simi dume suruwali, nimeondoa uoga,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU.
Nguvu zote zi mwilini, hadi zile za ziada
Bora niwe kwa makini, niutowe ushuhuda
Uridhike kwa mizani, uzito silete shida,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU.
Hichi kipya cha walili, watatu ufaidini,
Nitaufanya ukali, asibaki mlangoni,
Nyuki nile na hasali, juu wala sio chini,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU
Wakufumbua fumbua, lengo lidhiirike,
Watu pate yatambua, kila moja shike yake,
Mi mgongo nananyua, mwenyewe nipatoreke,
KUMBE MCHUZI WA PWEZA, UTAMU UZIDI HAMU
Wasaalamu
Wiseman Abubakar Mwaphombo
@002

Comments
Post a Comment