Ni furaha tele tele,pamoja tushangilie
Walipo popote pale,shangwe mama asikie
Sherehe pamoja tule,siku yao 'furahie
Tusimdharau mama!
Insi wote duniani,wote katoka kwa mama
Miezi tisa jamani,alivumilia mama
Tangu wetu utotoni,katulea sote vyema
Tusimdharau mama!
Mwalimu wa kwanza mama,yote mema kafundisha
Hakuchoka katu mama,penzi lake kazidisha
Mambo yote yale mema,katia sana puresha
Tusimdharau mama!
Na aliye kama mama,Mikaeli sijamwona
Hakika hakati tama,hamtelekezi mwana
Kinagaga nasema,mama ni kama Rabana
Tusimdharau mama!
Beti tano nikitua,nakuomba tafadhali
Furusa hii chukua,mzawadi tafadhali
Atakuombea dua,baraka zake Jalali
Tusimdharau mama!
MTUNZI: MICHAEL COSMAS
+254751388636
michaelcosmas96@gmail.com

Comments
Post a Comment