Hisani ya pixabay.com
Semi mdomo husemi,leo kalamu yatema,
Wala haina ugomi,leo mama kumsema,
Kweli siku haziyemi,miaka imeandama,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea,
Kweli maana ya mama, waijuao wenyewe,
Kamusini tutasoma,bado tusiwaelewe,
Tujaribu kutazama,vitendo vyao twelewe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea,
Yaini tulidondoka,bada miezi tisia,
Vifaranga ndo kufika,duniani twaingia,
Hatujui kujiruka,kwenu tulijifunzia,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea
Kufoka 'litufokea,hilo hatuwezi pinga,
Mateke yakatembea,miili mkairanga,
Tulihisi 'tuonea, ila ndo mlitujenga,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Kwa kucha mlichakura,kutwa tuyapate lishe,
Kazi bila mshahara,'liziita mishe mishe,
Japo ni kwa mutura,'lihustle mtulishe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Baridi hatukufili,mama mkiwa jawabu,
Joto lisilo mithili,nyie ndo mkawa blabu,
Malezi yalo kamili,mlitupa bila jibu,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Mgongoni tigatiga,waendana na mwanao,
Mashamba twayavuruga,kitoka hadi machweo,
Imradi tupate mega,kiazi na kitoweo,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
'Mekuwa wetu walinzi,kutokana wezi mwewe,
Humkujali majonzi,mbawa zenu zichaniwe,
Bilashaka 'lituenzi,kutulinda tusiliwe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea
Kwenu 'mejifunza mengi,ya akhera na dunia,
Twajua 'mefeli mengi,ila bado ipo nia,
Twaitafuta shilingi,kama 'livyotuambia,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Hapa ndipo twapumua,maji tuyapige tama,
Hatutachoka 'sifia,hulka zenu kina mama,
Leo twawasalutia,waja wote dunia nzima,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Athuman mdigo
Gwiji wa mashairi
Semi mdomo husemi,leo kalamu yatema,
Wala haina ugomi,leo mama kumsema,
Kweli siku haziyemi,miaka imeandama,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea,
Kweli maana ya mama, waijuao wenyewe,
Kamusini tutasoma,bado tusiwaelewe,
Tujaribu kutazama,vitendo vyao twelewe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea,
Yaini tulidondoka,bada miezi tisia,
Vifaranga ndo kufika,duniani twaingia,
Hatujui kujiruka,kwenu tulijifunzia,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea
Kufoka 'litufokea,hilo hatuwezi pinga,
Mateke yakatembea,miili mkairanga,
Tulihisi 'tuonea, ila ndo mlitujenga,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Kwa kucha mlichakura,kutwa tuyapate lishe,
Kazi bila mshahara,'liziita mishe mishe,
Japo ni kwa mutura,'lihustle mtulishe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Baridi hatukufili,mama mkiwa jawabu,
Joto lisilo mithili,nyie ndo mkawa blabu,
Malezi yalo kamili,mlitupa bila jibu,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Mgongoni tigatiga,waendana na mwanao,
Mashamba twayavuruga,kitoka hadi machweo,
Imradi tupate mega,kiazi na kitoweo,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
'Mekuwa wetu walinzi,kutokana wezi mwewe,
Humkujali majonzi,mbawa zenu zichaniwe,
Bilashaka 'lituenzi,kutulinda tusiliwe,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea
Kwenu 'mejifunza mengi,ya akhera na dunia,
Twajua 'mefeli mengi,ila bado ipo nia,
Twaitafuta shilingi,kama 'livyotuambia,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Hapa ndipo twapumua,maji tuyapige tama,
Hatutachoka 'sifia,hulka zenu kina mama,
Leo twawasalutia,waja wote dunia nzima,
Shukrani kina mama,vifaranga kutulea.
Athuman mdigo
Gwiji wa mashairi

Comments
Post a Comment