Bismillah Raufu, Mola aliyetukuka,
Sinalo la kukashifu, kasema litaumbuka,
Leo hai kesho mfu, katuumba Yah Rabuka,
Naitafuta zawadi, niweze mlipa mama,
Tatu haki mama twaa, nne yake yeye baba,
Nipate nuru ya taa, laana ndio msiba,
Mama naomba nufaa, nisijidunge na mwiba,
Naitafuta zawadi, niweze mlipa mama
Kila kona natafuta, lakini sijaona,
Machozi yangu nafuta, namuomba Rabana,
Sitaki mie kujuta, nikaikosa jahana,
Naitafuta zawadi, niweze mlipa mama
Nashukuru ni mzima, afia nguvu anazo,
Aniiti kunituma, wala sinao mzozo,
Namtendea mema, kwake sina ya likizo,
Naitafuta zawadi, niweze mlipa mama
Mama leo samahani, hadharani nayasema,
Sipo kuona machoni, baridi wangu mtima,
Ila furaha moyoni,nakupenda sana mama.
Naitafuta zawadi,niweze mlipa mama.
By Wiseman Abubakar
+254783101884

Comments
Post a Comment